Kaimu Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoani Mtwara, ACP Isack Mushi amesema Jeshi hilo linafanya uchunguzi wa matukio mawili ya vifo vya watoto wawili wanaodaiwa kujinyonga ambapo mmoja alichukua hatua hiyo baada ya kuzuiwa na kaka yake kwenda kuangalia video usiku kwenye mabanda.
Ameyasema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari ambapo amesema msichana huyo ambaye ni mwanafunzi wa shule ya sekondari Kilomba iliyopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Mtwara amekutwa amefariki baada ya kujinyonga chumbani kwake kwa kutumia mtandio wake.
Tukio hilo lilitokea Februari 26, 2023 majira ya saa sita usiku katika kijiji cha Muungano Kata ya Kiromba mkoani humo.