Abiria wanusurika kifo Pwani

Abiria waliokua wanasafiri na basi la Happy Nation lililokua likitokea mkoani Kagera kuelekea Dar es salaam wamenusurika kifo kufuatia gari hilo kupata ajali katika eneo la Vigwaza Mlandizi mkoani Pwani.

Mkuu wa mkoa wa Pwani Alhaj Aboubakar Kunenge amewatembelea majeruhi waliokimbizwa kwa dhararura katika hospitali ya Tumbi iliyopo Kibaha ambapo amesema ajali hiyo imetokea baada ya basi hilo kupinduka eneo la Vigwaza majira ya saa nane usiku wa kuamkia leo na hakuna aliyepoteza maisha

Kunenge amewataka madereva kufuata sheria ya usalama barabarani

Naye Mganga mfawidhi wa hospitali ya Tumbi Dk. Aman Malima amesema wameendela kupokea majeruhi kufuatia jali hiyo na kwamba majeruhi wote waliofikishwa hospitalini hapo wanaendelea vizuri



Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii