Rais Samia awatakia Kwaresma njema Wakristo wote

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amewatakia Kwaresma njema Wakristo wote nchini.

”Nawatakia Kwaresma njema Wakristo wote. Katika hija hii ya kiroho mnayoianza leo kwa Jumatano ya Majivu, endeleeni kuiombea nchi yetu na Dunia nzima amani na upendo. Majivu katika paji la uso yawakumbushe ubinadamu wenu na kumrudia Mwenyezi Mungu, mkiomba ulinzi wake kwetu sote.”- Rais Samia Suluhu Hassan

Leo ni Jumatano ya Majivu, ambapo waumini wa dini ya Kikristo katika mataifa mbalimbali duniani wanaungana kuanza mfungo wa Kwaresma.

Kwaresma ni mfungo wa siku 40, ambao utamalizika kwa adhimisho la sikukuu ya Pasaka ambayo ni kumbukizi ya mateso, kifo na ufufuko wa Yesu Kristo.


Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii