Wanafunzi katika chuo kikuu cha Maseno wamefanya maandamano kufutia kifo cha mmoja wao William Bhangi Mayenga mwanafunzi wa mwaka wa tatu aliyepigwa risasi shingoni na maafisa wa usalama.
Kifo cha Mayenga Jumatatu 20 nje mwa lango lango kuu la chuo hicho kimepelekea wanafunzi wa Maseno kuandaa mgomo wakidai haki kwa mmoja wao ipatikane.
Maafisa wa polisi wamekuwa na wakati mgumu wa kuwatuliza wanafunzi waliojawa na hamaki na waliotaka kumtendea haki Mayienga aliyefariki wakati wa maandamano yaliyoiitishwa na mrengo wa Azimio.
Maandamano ya leo yalianzia ndani mwa shule ambapo wanafunzi walikusanyika kusemezana kabla ya kuanza vurugu na maafisa wa usalama waliosimama kidete kuhakikisha kuwa utulivu unarejeshwa.