Wanaume wawili kutoka nchini Kenya wamepanda mti wakiwa uchi muda wa usiku Alhamis March 16 huku wakihubiri lakini waafisa wa usalama walifanikiwa kuwafuykuz watu hao.
Ijumaa asubuhi, wanaume hao walifanikiwa kufika eneo hilo na kupanda juu ya mti huo wakiwa uchi na kuanza kuhubiri.Maafisa wa polisi walizingira eneo hilo baada ya juhudi zao za kuwataka wanaume hao kuvaa nguo na kushuka mti huo kugonga mwamba.
Bila kutoa masharti yoyote, wanaume hao walionekana wakiwa wamebeba Bibilia na kuzungumza baina hayo huku polisi wakiendelea kuwaomba wateremke.Katika video hiyo ambayo imesambaa, wanaume hao wanasikika wakihubiri kwa kusema "Yesu ni Bwana" huku umati ukitazama kwa mshangao.