ELON MUSK HANA AMANI NA MTANDAO WA TWITTER

Kwa mujibu wa Mhandisi wa Twitter amesema Mfanyabiashara huyo anayemiliki Kampuni za #SpaceX, #Tesla, Twitter, #Neuralink na #TheBoring hutembea na Walinzi 2 kila anapofika #TwitterHQ.


Mfanyakazi huyo amesema #ElonMusk Ameonesha kuwa na hofu juu ya Usalama wake na hana imani na Wafanyakazi wa #Twitter. Pia, Elon amekuwa akiwatumia Wahandisi wa Tesla katika kutathmini uwezo wa Wahandisi wa Twitter ili kubaini wanaopaswa kufukuzwa kazi.


Mbali na Elon kuwa na Walinzi kila mahali, Business Insider wameripoti kuwa #MarkZuckerberg, Bosi wa #META inayoendesha mitandao ya #Facebook, #WhatsApp na #Instagram ametengewa bajeti ya Tsh. Bilioni 32.7 kwa mwaka 2023 kwaajili ya Ulinzi wake na familia yake


Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii