9 wafariki ajalini Katavi, 30 wajeruhiwa

Watu tisa wamefariki na wengine 30 wamejeruhiwa kwa  ajali iliyotokea katika Mlima mkali wa Nkondwe, Halmashauri ya Wilaya ya Tanganyika Mkoa wa Katavi.

Ajali hiyo imehusisha basi (Tata) lenye namba za usajili T506 DHH kampuni ya Komba's ambalo limepinduka na kudondokea bondeni

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Katavi Ali Makame amesema ajali hiyo imetokea March 6, 2023 jioni 
“Baada ya kufika katika Mlima huo gari liliserereka na kudondokea kwenye bonde kubwa lenye kina cha Mita zisizopungua 75” amesema Kamanda Makame

Kwa mujibu wa  Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Wilaya ya Tanganyika Dk. Alex Mrema amesema vifo hivyo tisa vimetokea papohapo ambapo kati ya waliofariki Wanaume ni watano na Wanawake ni wanne akiwemo mjamzito
Jeshi la Polisi mkoani humo linaendelea na uchunguzi huku zoezi la kuitambua miili likiendela kwa ajili ya taratibu nyingine.


Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii