Mwanamke mwingine akutwa amekufa Arusha

Mwanamke mwingine mkazi wa Njiro jijini Arusha, Janerose Dewasi (66) amekutwa amefariki dunia nyumbani kwake baada ya kupigwa na kitu chenye ncha kali.

Tukio hilo limetokea siku chache baada ya mfanyabiashara wa madini ya Tanzanite, Ruth Mmassy anayedaiwa kuuawa na mtoto wake

Kamanda wa Polisi Mkoani Arusha, Justine Masejo amethibitisha kutokea tukio hilo leo Jumatano Desemba 29, 2021 na kueleza kuwa wanamsaka mfanyakazi wa ndani ambaye  alikuwa anaishi na marehemu huyo.

Kamanda Masejo amesema mwili wa mwanamke huyo aliyekuwa anaishi na mfanyakazi wa ndani kwenye nyumba yake eneo la block D amekutwa amepigwa na kitu chenye ncha kali kwenye paji la uso huku akibainisha kuwa Jeshi la Polisi linamsaka mfanyakazi wa ndani ambaye anadaiwa kutoroka muda mfupi kabla ya kugundulika tukio hilo.

"Uchunguzi wa awali umebaini kuwa marehemu alikuwa anaishi na mtumishi wa kazi za ndani ambaye alianza kazi wiki moja iliyopita" amesema

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii