Takriban Wafugaji 27 wameuawa na wengine kadhaa kujeruhiwa baada ya
kutokea mlipuko wa bomu katika eneo lenye mivutano ya kikabila na
kidini nchini Nigeria.
Kwa mujibu wa Kamishna
wa polisi wa Nasarawa, Maiyaki Muhammed Baba amesema Wafugaji hao, ambao
walikuwa wakichunga mifugo, walikuwa katika kijiji cha Rukubi kilichopo
kwenye mpaka kati ya majimbo ya Nasarawa na Benue.
Moja kati ya matukio ya mauaji ambayo yaliwahi kutokea nchini Nigeria. Picha ya The Telegraph.
Amesema,
“Tumegundua watu 27 waliuawa katika mlipuko wa bomu pamoja na ng’ombe
kadhaa, alisema na watu wengi walijeruhiwa na idadi ya vifo inaweza
kuongezeka na tayari wataalam wa mabomu wameanza kuchunguza chanzo cha
mlipuko huo.”
Chama kinachowakilisha wafugaji,
kimesema mlipuko huo ulisababishwa na shambulizi la anga la kijeshi,
huku kukiwa hakuna taarifa za kundo lolote la uasi lililodai kuhusika na
shambulio hilo lililoacha simanzi na vilio kwa jamaa za marehemu.
Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii