mapigano ya kikabila Ethiopia yaua raia

Makabiliano hayo yaliibuka siku ya Jumamosi katika mji wa Jewuha lililopo jimbo la Amhara. Mmoja ya mashuhuda ambaye hakutaka kutambulishwa aliliambia shirika hilo la habari kwamba wanamgambo wanaodhaniwa kutoka Jeshi la Mapinduzi la Oromo, waliishambulia kambi iliyotumiwa na vikosi maalumu vya Amhara na kuwaua zaidi ya wanajeshi wake 20.

Shuhuda mwingine katika mji wa Ataye, katika jimbo la Amhara amedai kwamba mapigano kati ya OLA na vikosi hivyo maalumu vya Amhara yalikuwa yakiendelea na maelfu ya raia wamekimbia.

Serikali ya jimbo la Amhara imethibitisha jana kuhusu mapigano hayo na kusema wanajeshi wa jeshi la shirikisho, polisi na vikosi maalumu vya Amhara wanapambana kurejesha utulivu, huku wasemaji wa polisi ya shirikisho na serikali wakikataa kuzungumza


Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii