Mbwa Ampiga Risasi na Kumuua Mmiliki Wake Wakati wa Uwindaji

Katika kisa adhimu kuwahi kushuhudiwa ulimwenguni, mwanamume mmoja nchini Marekani anaripotiwa kupigwa risasi na mbwa wake walipokuwa mawindoni. 


Mbwa huyo anasemekana kufyatua risasi hiyo walipokuwa wakiendesha gari. Marehemu Wichita mwenye umri wa miaka 32, mkazi wa Kansas, aliuawa Jumamosi, Januari 21, kwa mujibu wa ripoti ya ofisi ya Sheriff wa Sumner County. Kulingana na ripoti hiyo, mbwa huyo alikanyaga bunduki alipokuwa ameketi kwenye kiti cha nyuma cha gari na kufyatua risasi iliyompata mmiliki wake. 
Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii