Mwalimu Aliyerekodiwa akichapa Watoto kwenye visigino Asimamishwa Kazi

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Adolf Mkenda amesema hatua stahiki zitachukuliwa dhidi ya Mwalimu aliyeonekana katika picha ya video iliyosambaa kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii akimuadhibu mwanafunzi kinyume na taratibu.

Profesa Mkenda amesema wameishafuatilia jambo hilo na tayari mwalimu huyo amesimamishwa kazi huku uchunguzi ukiendelea.


Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii