Mwanamume mmoja anadaiwa kupoteza nyeti zake kufuatia kichapo cha mbwa alichopokezwa katika maandamano ya kupinga mageuzi ya pensheni nchini Ufaransa.
Katika maandamano hayo ya Alhamisi, Januari 19, zinazosambaa mtandaoni, afisa wa polisi anaonyeshwa akimpiga mwanamume mmoja mateke katikati ya miguu, na kisha kuondoka.
Mwanaume huyo anaonekana akiwa ameshika kamera. Wakili wa mwanamume huyo Lucie Simon alisema Jumapili, Januari 22, kuwa atawasilisha malalamishi kwa niaba ya mteja wake ambaye ni mhandisi mwenye umri wa miaka 26.
Mwanamume huyo mwenye asili ya Kihispania anaripotiwa kwamba alikuwa akipiga picha za maandamano hayo kwa hiari na kupelekea kukatwa kwa nyeti zake na polisi.