Jeshi la polisi mkoani Iringa linawashikilia wafanyabiashara watatu wa maduka yaliyopo mkabala na ofisi za mamlaka ya mapato TRA ambayo yanajihusisha na vifaa vya maofisini kwa kushirikiana na baadhi ya maofisa wa TRA.
Kutoa leseni za udereva, kubadilisha kadi za umiliki wa vyombo vya moto bila kufuata utaratibu uliowekwa kisheria
Kamanda wa Jeshi la polisi mkoa wa Iringa ACP Allan Bukumbi amesema kuwakamatwa kwa watuhumiwa hao ni kutokana na kupata taarifa kutoka kwa wasamaria wema
Amesema walipokea taarifa kuwa maeneo ya mtaa wa Mahiwa kata ya Gangilonga Manispaa ya Iringa kuna wafanyabiashara wa maduka yanajihusisha na vifaa vya maofisini wanashirikiana na watumishi wawili wa TRA kutoa leseni na kuwapa wananchi bila kufuata utaratibu wa kisheria
Aidha kamanda Bukumbi amesema Jeshi hilo linaendelea kuwatafuta wenye leseni hizo za udereva na wamiliki wa namba za magari kwa kosa la kula njama na kujipatia leseni na namba bila kufuata mfumo uliowekwa kwa mujibu wa sheria
Watuhumiwa watafikishwa mahakamani upelelezi utakapokamilika