Tunarudi enzi za chama kimoja ‘Mtukufu Rais’

Kiongozi wa Azimio la Umoja, Raila Odinga amesema serikali tawala ya Kenya Kwanza inanuia kurejesha Kenya katika enzi za mfumo wa chama kimoja ambacho kilikuwepo wakati wa utawala wa Rais Moi.

Kupitia taarifa iliyoangazia maazimio yaliyotolewa wakati wa baraza la umma mjini Kisumu, Raila alidai kuwa hofu inayoenezwa na serikali inabana mafanikio waliyopata katika “haki na uhuru waliopigania”. 

Amesema, serikali inayoongoza inapuuza nia ya kuwa na uchaguzi na kwamba wanavifanya vyama vingine kuonekana havina maana.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii