Mwanasiasa wa upinzani nchini Cameroon, Issa Tchiroma Bakary amekimbilia nchini Gambia hii ikiwa ni kulingana na serikali ya Gambia siku ya Jumapili.
Tchiroma aliyegombea urais kwenye uchaguzi wa mwezi Oktoba na anayepinga matokeo ya uchaguzi huo uliomrejesha madarakani Rais Paul Biya, anaarifiwa kuingia Gambia tangu Novemba 7 kwa misingi ya kibinaadamu na kuhakikisha usalama wake.
Hatua hiyo imefikiwa huku majadiliano yakiendelea ya kusaka suluhu ya amani na kidiplomasia katika mvutano wa baada ya uchaguzi nchini Cameroon. Tchiroma anadai kushinda kwenye uchaguzi huo na mara kadhaa aliwahamasisha wananchi kuandamana kupinga matokeo hayo.
Serikali ya Cameroon imesema itamfungulia mashitaka kufuatia miito hiyo ya maandamano inayosimamisha shughuli za nchi.
#10YrsJembefm #Familiamoja #AhsantekwaTime