Mgombea huru adai kuibuka mshindi wa uchaguzi wa urais

Nchini Guinea Bissau mgombea huru Fernando Dias da Costa, anayeungwa mkono na chama cha Social Renewal Party (PRS) na Muungano wa kisiasa wa Terra Ranka amedai kushinda  duru ya kwanza  katika uchaguzi wa urais wa uliofanyika Jumapili.

Tangazo hilo linakuja siku moja baada ya tume ya uchaguzi nchini humo kusema uchaguzi huo ulikuwa mtulivu.

Dias da Costa ambaye ni mgombea huru na anayeungwa mkono na chama cha Social Renewal Party (PRS) na Muungano wa kisiasa wa Terra Ranka,aidha amesema ameshinda kiti hicho katika awamu ya kwanza na kutupilia mbali uwezekano wa kurudiwa kwa uchaguzi huo.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na tume ya uchaguzi nchini humo Uchaguzi huo uoliwashirikisha karibia wapiga kura 960,000 kumchagua rais na wabunge, ulifanyika kwa amani na utulivu lakini haukukosa changamoto ambazo zilitatuliwa kwa haraka.

Matokeo ya uchaguzi huo yanatarajiwa kabla ya tarehe 27 Novemba, ingawa sheria inaruhusu muda wa siku saba hadi kumi,wakati huu tume ya uchaguzi  ikiwataka  wapiga kura, vyama vya siasa na vyombo vya habari kutochapisha takwimu zozote kabla ya tangazo rasmi.

Uchaguzi huo unamshirikisha rais aliye madarakani Umaro Sissoco Embaló, anayewania muhula wa pili, dhidi ya wapinzani kumi na mmoja, akiwemo mtangulizi wake José Mário Vaz, anayejulikana kama Jomav, na waziri mkuu wa zamani Baciro Djá.

#10YrsJembefm  #Familiamoja #AhsantekwaTime

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii