Mhubiri amependekeza kuanzishwa kwa matoleo maalum makanisani ili kutakasa Hazina ya Kitaifa.
Pasta Wilfred Lai alikuwa miongoni mwa watumishi wa Mungu walioongoza ibada ya maombi ya taifa katika Uwanja wa Kitaifa wa Nyayo mnamo Jumanne, Februari 14.
Katika mahubiri yake, Lai aliwaomba mapasta wenzake kuomba 'Sadaka Takatifu' kutoka kwa waumini wao. Mwasisi huyo wa Kanisa la Jesus Celebration Centre (JCC) alidai kuwa uchumi wa Kenya umekuwa ukidorora kutokana na utawala uliopita kupuuza nguvu za Mungu.