Seneta wa Nigeria Ashtakiwa Uingereza kwa Njama ya Kuvuna Figo

Mwanasiasa tajiri kutoka nchini Nigeria na mkewe wanakabiliwa na mashtaka nchini Uingereza kwa kupanga njama ya kuvuna figo ya mchuuzi ili kumpandikiza binti yao.

Ike Ekweremadu, 60, ambaye ni seneta wa upinzani nchini Nigeria na pia naibu rais wa zamani wa seneti, na mke wake walikuwa "watu mashuhuri" katika jamii ya Nigeria.Ekweremadu na mkewe Beatrice Ekweremadu, mwenye umri wa miaka 56, binti yao Sonia mwenye umri wa miaka 25 na daktari Obinna Obeta, 50, wanadaiwa kula njama ya kutumia njia ya uwongo kumdhulumu mchuuzi mwenye umri wa miaka 21 ili kupata figo yake.



Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii