Kauli ya machifu kudai kuwa hautambui mamlaka imesababisha kuzuka kwa mapigano ya kugombania ardhi na watu 13 kuuawa na wengine 40 kujeruhiwa huko Las Anod, mji ambao unagombaniwa na vikosi vya Somaliland na Somalia.
Mapigano hayo, yalianza hapo alfajiri ya Februari 6, 2023 kati ya vikosi vya serikali vilivyoko karibu na mji huo na wapiganaji wa ndani, ikiwa ni siku moja baada ya tangazo la machifu wa kimila kudai hawaitambui mamlaka ya Somaliland.