Watu wasiopungua 9 wamepoteza maisha kufuatia mkanyagano uliotokea wakati wa sherehe za kuukaribisha mwaka mpya kwenye mji wa Uganda, Kampala. Polisi imesema mkanyagano uliotokea dakika chache baada ya ufyetuaji fashifashi za kuukaribisha mwaka kwenye viunga vya mtaa wa maduka na biashara wa Freedom City.Mbali ya watu tisa waliopoteza maisha, wengine 5 wamejeruhiwa na walipelekwa hospitali na waota msaada wa huduma za dharura.Sherehe za kuukaribisha mwaka mpya 2023 zilikuwa za kwanza kufanyika kwenye taifa hilo la Afrika Mashariki baada ya kuitishwa kwa miaka mitatu kutokana na vizuizi vya kupambana na janga la corona na sababu za kiusalama.