Takriban watu 60 wameuwawa katika ghasia huko Sudan Kusini

Takriban watu 60 wameuwawa wengi wao wakiwa wanawake na watoto kwenye migogoro katika eneo la utawala la Greater Pibor huko mashariki mwa Sudan Kusini.

Watu wengine 20 walijeruhiwa siku ya Jumapili katika shambulio jingine lililofanywa na mamia ya wanamgambo katika jimbo la Jonglei huko Greater Pibor.

Waziri wa habari katika eneo hilo Abraham Kelang Jiji amesema, makundi ya wanakijiji yalisherehekea Krismasi wakiwa wamejificha vichakani bila chakula na kulitaja shambulio hilo kama la kinyama.

Ghasia zimekuwa zikizuka mara kwa mara katika wiki za hivi karibuni kwenye majimbo ya Jonglei na Upper Nile mashariki mwa nchi.

Vita vya wenyewe kwa wenyewe vilizuka mnamo 2013, ambapo maelfu walikufa na mamilioni walikimbia makaazi yao katika taifa hilo lenye utajiri wa mafuta lililojipatia uhuru wake mwaka 2011.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii