Watu 5 wamefariki dunia papo papo Mikumi Wilayani Kilosa Mkoani Morogoro katika ajali iliyohusisha gari ndogo maarufu kama "IT" iliyokuwa ikitokea Bandarini Jijini Dar-es-salaam kuelekea mpakani Tunduma baada ya kugongana uso kwa uso na gari kubwa la mafuta aina ya Benzi iliyokuwa ikitokea Mkoani Iringa kuelekea Mkoani Morogoro.
Akithibitisha ajali hiyo, Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Morogoro FORTUNATUS MUSILIMU amesema ajali hiyo iliyotokea majira ya usiku wa kuamkia Jumatatu eneo la IYOVI wilayani Kilosa Mkoani Morogoro katika barabara kuu ya Morogoro-Iringa na kusema imesababishwa na uzembe wa dereva wa wa gari ndogo ambaye inasemekana alikuwa akiendesha kwa kasi na gari likamshinda katika kona na kuvamia lori hilo.