Mamlaka ya kisiwa cha Taiwan imesema China ilipeleka ndege 71 za kivita katika eneo la ulinzi la kisiwa hicho katika muda wa saa 24 hadi jna Jumatatu. Kwa upande wake, China ilisema ndege hizo zilikuwa sehemu ya ''luteka za mashambulizi'' na jibu kwa ilichokieleza kuwa ni ''uchokozi na kuzidisha mivutano'' vinavyofanywa na Marekani pamoja na Taiwan.
Beijing imesema imekasirishwa na hatua ya bunge la Marekani kuweka fuko linalohusu Taiwan katika bajeti ya ulinzi ya Washington iliyopitishwa Jumamosi. Kinachojulikana kama ''luteka za mashambulizi'' mara hii kilikuwa cha juu kabisa kuwahi kufanyika katika anga ya Taiwan kwa siku moja.
Taiwan ilisema kuwa ndege 43 za China zilivukwa mstari wa baharini unaokitenganisha kisiwa hicho na China Bara, ambao ni mpaka usio rasmi baina yao.
Mamlaka ya Taiwan imesema iliweka mfumo wake wa ulinzi wa makombora katika tahadhari ya hali ya juu.