Aliyekuwa Seneta wa Lamu Avamiwa, Kuporwa Akielekea Gestini Ngara

Aliyekuwa seneta wa Lamu Anwar Loitiptip anauguza majeraha baada ya kushambuliwa na kuibiwa alipokuwa akielekea katika nyumba yake ya wageni huko Ngara. 

Mbunge huyo wa zamani ambaye alihudumu katika kiti cha useneta wa Lamu kati ya 2017 na 2022 alivamiwa na majambazi katika mzunguko wa Globe Cinema jana usiku. 

Mbunge huyo wa zamani ambaye alihudumu katika kiti cha useneta wa Lamu kati ya 2017 na 2022 alivamiwa na majambazi katika mzunguko wa Globe Cinema jana usiku. 

"Majambazi waliomvamia kabla ya kumpokonya simu yake ya rununu na vitu vingine vya thamani walitoweka muda mfupi baadaye kuelekea Nairobi River, na kumwacha Seneta huyo akihangaika," DCI ilisema. 

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii