Gambia kuomboleza kwa siku saba

Rais wa Gambia Adama Barrow ametangaza siku saba za maombolezo kufuatia kifo cha Makamu wa Rais Badara Alieu Joof akiwa na umri wa miaka 66.


Bwana Joof alifariki nchini India baada ya kuugua kwa muda mfupi.

Inasemekana alikuwa akipokea matibabu huko, lakini serikali haijathibitisha hilo.Mara tu mwili wake utakaporejea, utalala bungeni hadi mazishi yake.Hakuna tarehe rasmi  iliyopangwa kwa ajili ya maziko yake.

Taarifa ya serikali ilimtaja Bw Joof kama "msomi wa akili kubwa", na "raia mwaminifu wa Gambia ambaye alitumia maisha yake yote kujaribu kuboresha wanadamu wengi".


Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii