Wanufakia mikopo Elimu ya Juu kuongezeka

Waziri wa Elimu, Prof. Adolf Mkenda leo, amesema ili kuwezesha na kuimarisha huduma ya utoaji na upatikanaji wa mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu wenye sifa na uhitaji Serikali itaongeza fursa za mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu kutoka 223,201 hadi 252,245.

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Mhe. Prof. Adolf Mkenda amesema Serikali itaendelea na ujenzi wa vyuo 65 vya mafunzo ya ufundi stadi, kati ya hivyo 64 ni vya wilaya na kimoja ni cha ngazi ya Mkoa wa Songwe.


Akizungumza wakati wa uwasilishaji wa bajeti ya wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2024/25 ameeleza kuwa Serikali imeongeza vifaa vya kufundishia na kujifunzia katika vyuo 29 vilivyokamilisha ujenzi.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii