Aliyempofua mchumba kwa Tindikali jela miaka 30

Mohamed Mwarandu Kombe (30), amehukumiwa miaka 30 jela baada ya kupatikana na hatia ya kummwagia tindikali usoni aliyekuwa mchumba wake, Fatma Kaingu (23).

Hukumu hiyo, imetolewa na Mahakama ya Mombasa Nchini Kenya baada ya mshitakiwa kupatikana kosa hilo lililomsababishia Fatma kuwa kipofu.

Hakimu mkaazi Mwandamizi wa Mahakama hiyo, Gladys Olimo amesema amezingatia ushahidi uliotolewa na upande wa mashtaka, na ule wa mlalamikaji ulioambatana na ripoti za matibabu.

Katika ushahidi wa kitabibu, Madaktari walisema macho yake yaliharibika zaidi na hivyo kupoteza uwezo wa kuona na kwamba haingewezekana kumtibia kutokana na jinsi yalivyoathiriwa na kemikali hiyo.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii