Israeli imefungua tena mpaka wa Kerem Shalom kuruhusu misaada kuingia Gaza

Washirika wa Israeli wamekuwa wakionya dhidi ya oparesheni zake katika eneo la Rafah lenye idadi ya raia wa Palestina zadi ya milioni moja wengi wao ambao walitoroka mapigano yanayoendelea kati ya Hamas na wanajeshi wa Israeli katika maeneo mengine.

Israeli inasisitiza kuwa Rafah ndio eneo peke ambalo wapiganaji wa Hamas wangali wanajificha na kwamba inahitaji kumaliza kundi hilo na washirika wake.

Marekani ilisitisha mpango wake wa kutuma mabomu nchini Israeli wiki iliopita kutokana na hofu kuwa mshirika wake alikuwa anakaribia kutekeleza oparesheni za kijeshi katika eneo la Rafah.


Marekani, Misri na nchi yake Qatar ambao ni wapatanishi wakuu katika mzozo wa Hamas na Israeli wanaendelea na juhudi zao za kuafikia suluhu ya usitishaji wa mapigano katika ukanda wa Gaza.


Mpaka wa Rafah umekuwa muhimu kwa mashirika ya kutoa misaada tangu mapigano kuzuka na ndilo eneo peke ambalo raia wanaweza kuingia na kuondoka Gaza.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii