ambalo limeshuhudia mamia ya watu wakifariki katika ajali za ndege katika miongo ya hivi karibuni.
Kwa miaka mingi, sababu kadhaa zimelaumiwa kwa rekodi mbaya ya usalama ya mashirika ya ndege ya Nepal. Mandhari ya mlima na hali ya hewa ambayo mara nyingi haitabiriki inaweza kuwa gumu kutabiri, na mara nyingi hutajwa kama sababu. Lakini wengine wanataja ndege zilizopitwa na wakati, kanuni zilizolegea na uangalizi mbaya kama mambo yanayochangia ajali hizo.
Bado haijafahamika ni nini kilisababisha ajali hiyo ya Jumapili.