Mali yasema wanajeshi wake 14 wameuwawa katika mashambuli mawili ya wanamgambo

Wanajeshi 14 wa Mali wameuwawa na wengine 11 wamejeruhiwa katika mashambulzii mawili tofauti yaliyotokea katikati mwa nchi hiyo baada ya magari waliyokuwa wakitumia kukanyaga mabomu. Hayo yameelezwa na jeshi la taifa jana Jumatano.

Matukio hayo mawili yametokea kwenye mikoa ya katikati mwa Mali ambako wanamgambo wenye mafungamano na makundi ya itikadi kali ya Al-Qaeda na lile linalojiita Dola la Kiisamu, hufanya mashambulizi ya kila wakati yakiwalenga raia na vikosi vya usalama.

Hadi sasa hakuna kundi lilodai kuhusika na mashambulizi hayo. Jeshi la Mali limesema kufuatia mkasa huo lilituma kikosi cha ziada kufanya operesheni iliyowaua wanamgambo 31.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii