Mmiliki wa Mochari Asukumwa Jela Miaka 20 Kwa Kuuza Viungo vya Miili 560

Mmiliki wa zamani wa makafani katika Jimbo la Colorado, Marekani, amehukumiwa kifungo cha miaka 20 gerezani kwa kuwalaghai jamaa za waliofariki na kuuza viungo vya miili ya maiti 560 bila idhini.


Megan Hess, 46, aliungama makosa ya ulaghai mnamo Julai 2022, akiendesha hifadhi ya maiti ya Sunset Mesa.


Hess pia alikuwa anamiliki shirika la kutoa huduma za mchango wa viungo vya mwili kutoka jengo moja mjini Montrose, Colorado.Alihukumiwa kifungo cha miaka 20 mnamo Jumanne, Januari 3, ambacho ndicho kinruhusiwa chini ya sheria ya taifa hilo.

Mamake Hess, mwenye umri wa miaka 69, Shirley Koch, pia alikiri kosa la ulaghai na alihukumiwa kifungo cha miaka 15.

Mahakaa iliambiwa kuwa jukumu kuu la Koch lilikuwa kukatakata miili.




Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii