WATANZANIA WAASWA KUILINDA AMANI YA NCHI YAO

Mufti Mkuu wa Tanzania shehe Abubakari Zuberi amewatahadharisha watanzania kuilinda amani ya nchi yetu kwamba ikiondoka kuirudisha itachukua muda mrefu.

Amesema hayo katika Maulidi ya kumswalia mtume iliyofanyika katika viwanja vya shule ya msingi Mkuranga Wilayani Mkuranga mkoani Pwani nakuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa dini ya kiislam kutoka nchi za uarabuni, Uingereza, Lamu mjini Mombasa nchini Kenya, mashehe kutoka mikoa ya Dar es salaam na uongozi wa Bakwata mkoa wa Pwani na wilaya ya Mkuranga sambamba na uongozi wa chama na serikali ngazi ya wilaya ya Mkuranga.

Amesema amani iliyopo katika nchi yetu ikiondoka inaweza kuchukua hata miaka 50 kurudi tena katika nchi yetu na kwamba wengi wetu inawezekana hatutakuwepo kipindi hicho.

"Amani tuliyonayo tukiichezea ikatoweka na ikitoweka hairudi mapema inaweza kuchukua miaka mingi hata miaka 50 sisi sote tunaweza tukawa hatupo kipindi hicho Kwa sababu kitu tunacho tunakichezea kama vile amani"



Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii