MWILI WA ASKOFU KWANGU WAOKOTWA UKIELEA ZIWA VICTORIA

Askofu mstaafu wa Kanisa la Anglikana Tanzania Dayosisi ya Victoria Nyanza (DVN), Boniphace Kwangu (61) amekutwa amefariki dunia katika mazingira ya kutatanisha.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Wilbroad Mutafungwa amethibitisha kutokea kwa tukio hilo akisema kuwa, marehemu aliaga  familia  yake  na  kuelekea  wilaya  ya Sengerema kwa ajili ya kupokea malipo ya mwisho ya shilingi 2,500,000/=  baada ya kuwa ameuza eneo lake pamoja na nyumba kwa kanisa la KKKT- Sengerema. 

Hata  hivyo  hakuweza  kulipwa  kiasi  hicho  cha  fedha  kwa  kuwa  wanunuzi walimtaka awasilishe nyaraka ya umiliki wa eneo hilo hivyo, alirudi Mwanza mjini kwa ajili ya kushughulikia nyaraka hizo. 

Ilipofika  jioni ya siku hiyo familia yake walipata wasiwasi kuhusu alipo Boniphace  William Kwangu  kwani  hakuwa  amerudi  nyumbani  pia  alikuwa hapatikani kwenye simu  yake  ya mkononi.   

Kutokana na hali hiyo ilibidi familia yake watoe taarifa Kituo cha Polisi Kirumba.

Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza kwa kushirikiana na familia na watu mbalimbali lilianza  kufanya  ufuatiliaji  ili  kubaini  alipo  askofu. ZAIDI VIDEO



Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii