Mbunge Amtandika Mwenzake Bungeni

Kizaazaa kilizuka katika Bunge la Kitaifa nchini Senegal siku ya Alhamisi, Disemba 1, baada ya mbunge wa kiume kumtandika mwenzake wa kike kichwani.
Tukio hilo lilitokea wakati wa uwasilishaji wa bajeti baada ya mbunge wa upinzani Massata Samb kuondoka jukwaani na kuelekea kwa Amy Ndiaye Gniby wa muungano tawala wa Benno Bokk Yakaar na kumpiga.


Kutokana hasira, Gniby aliamua kulipiza kisasi kwa kumrushia kiti Samb, kabla ya wabunge wengine kuingilia kati kutuliza hali hiyo.
Samb aliikumbusha Bunge kuhusu matamshi ambayo Gniby alikuwa ametoa hapo awali ambayo aliyataja kama yasiyokuwa na adabu.


Akionekana kujibu kwa kiburi, Gniby anasemekana kutoka kwenye kiti chake na kusema kwamba "hakujali" kisha Samb naye alikatisha hotuba yake na kukimbilia kwake kumpiga

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii