Watu wasiopungua 488 wameuawa katika maandamano Iran

Shirika linalochunguza haki za binadamu nchini Iran limesema watu 488 wameuawa na maafisa wa usalama katika kukandamiza maandamano yaliyozuka baada ya kifo cha msichana Mahsa amini, aliyekufa mikononi mwa polisi wa maadili mwezi Septemba.

Kwa mujibu wa ripoti ya shirika hilo iliyochapishwa jana Jumanne, nusu ya wahanga waliuawa katika maeneo yenye wakaazi wengi wa jamii za Wakurdi na Wabaloch. Katika mkoa wa Sistan-Baluchistan ambao wakaazi wengi ni wa madhehebu ya Suni, ripoti hiyo imesema watu 128 waliuawa, ikiwa idadi kubwa zaidi ya vifo katika mkoa mmoja. Mamlaka za Iran kwa mara ya kwanza zimekiri kuwa watu zaidi ya 300 wamepoteza maisha katika ghasia hizo.

Wiki iliyopita, baraza la haki za binadamu la Umoja wa Mataifa liliunga mkono kuanzishwa kwa uchunguzi katika unyanyasaji dhidi ya waandamanaji nchini Iran.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii