O Yeong-su ashtakiwa kwa unyanyasaji wa kingono

Muigizaji wa Squid Game, O Yeong-su amefunguliwa mashtaka ya unyanyasaji wa kingono kitendo alichofanya mwaka 2017.

Mwendesha mashtaka wa Korea Kusini amesema kuwa, O Yeong-su mwenye umri wa miaka 78 anatuhumiwa kwa kumgusa isivyofaa mwanamke mmoja mwaka 2017.

O Yeong-su mwezi Januari alitangazwa kama Mkorea Kusini wa kwanza kutwaa tuzo ya Golden Globe.


Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii