Majambazi Wavamia Kanisa Wakati wa Ibada na Kupora Waumini

Waumini wa kanisa la SDA jijini Johannesburg walipoteza vitu vya thamani ikiwemo pesa taslimu wakati wa ibada ya kanisani
Ripoti zinaonyesha kuwa wanaume sita waliokuwa wamejihami na bunduki walivamia kanisa hilo huku mhubiri akitoa mahubiri kwenye mimbari.
 Kulingana na taarifa ya uongozi wa kanisa hilo, tukio hilo lilinaswa kwenye kanda iliyokuwa ikipeperusha ibada hiyo moja kwa moja siku ya Jumamosi.Mhubiri wa kanisa hilo ambaye kwa hakika anaonekana alikuwa na hofu iliyomvaa usoni mwake, alikwenda kuketi baada ya majambazi kumkatiza akieneza injili.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii