Mkeka wa Drake wachanika

Rapper Drake ameliwa kiasi cha dola za kimarekani milioni moja katika mchezo wa betting baada ya kuipa ushindi Argentina kuifunga Ufaransa ndani ya dakika 90.

Staa huyo wa muziki kutoka nchini Canada alishuhudia akipoteza kiasi hicho cha pesa baada ya mchezaji Kylian Mbappe kuipatia goli la pili Ufaransa na kuufanya mchezo huo kumalizika kwa sare ya goli 2-2 katika uwanja wa Lusail.

Drake ambaye alikuwa akishabikia timu ya taifa ya Argentina picha zake ziliibuka mitandaoni akiwa amevalia jezi za Klabu ya Napoli akitangaza kuiunga mkono Argentina kwenye fainali hiyo ya Kombe la Dunia.

Miezi iliyopita staa huyo wa muziki aliliwa kiasi cha dola za kimarekani milioni mbili baada ya kumpa ushindi Bingwa wa zamani wa UFC Israel Adesanya kuutetea mkanda wake dhidi ya  Alex Pereira na matokeo yake akapigwa

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii