Karibu watu 19 wamekufa baada ya lori la mafuta kuanguka na kushika moto nchini Afghnaistan huku wengine 30 wakijeruhiwa vibaya, taarifa hii ikiwa ni kulingana na maafisa jana Jumapili. Maafisa hao wamesema lori hilo lililipuka baada ya kupinduka na baadae kushika moto ambao pia ulisambaa kwenye magari mengine.
Afisa wa afya katika mji wa Parwan Abdullah Afghan Mal amesema haikuwa rahisi kugundua miili ya waliofariki iwapo walikuwa ni wanaume ama wanawake kutokana na kuungua vibaya. Msemaji wa serikali ya Taliban Qari Yusuf Ahmadi amesema wametuma salama za pole kwa familia za wahanga na imetoa mwito kwa mashirika yanaohusika kufanya jitihada za kuzuia kutokea tena kwa ajali kama hizo.