Polisi wako macho baada ya kupokea ripoti za ujasusi zinazobainisha kwamba kundi la kigaidi la al-Shabaab, linapanga misururu ya mashambulizi wakati wa msimu wa sikukuu ya Christmas.
Kamanda wa Kaunti ndogo ya Madaraka Timothy Odingo amesema kwamba wanamgambo wa al-Shabaab wanapanga mashambulizi jijini Nairobi ili kuvuruga shamrashamra za siku kuu.
Kwa mujibu wa 'internal memo' Odingo, ametaka usalama kuimarishwa pamoja na watu kuwa makini ili kutibua mashambulizi hayo.
Maeneo yanayoaminika kulengwa na kundi hilo la kigaidi ambalo asili yake ni Somalia ni pamoja na Presbyterian Guest House na Conference Centre mtaani South C na Our Lady Queen of Peace Catholic Church mtaani South B.
Odingo ametoa wito kwa amaafdisa wa usalama kutumwa katika maeneo hayo yaliyotajwa ili kushika doria, kuweka vizuizi na kukagua magari pamoja na kupiga doria.