Mtoto Wa Aliyekuwa Rais wa Msumbiji Afungwa Jela Miaka 12 kwa Wizi

Mahakama ya Msumbiji imemhukumu mwana wake aliyekuwa rais wa taifa hilo Armando Guebuza kifungo cha miaka 12 jela kwa kuhusika katika kashfa ya rushwa.


Ndambi Guebuza, na wakuu wawili wa zamani wa ujasusi, Gregorio Leao na Antonio do Rosario, walihukumiwa kifungo cha miaka 12 jela kila mmoja.

Akitoa uamuzi huo, Jaji Efigenio Baptista alisema uhalifu uliofanywa na watatu huo umeleta madhara ambayo yatadumu kwa vizazi nchini humo.Katika kesi hiyo, jumla ya watu 19 walifunguliwa mashtaka ya ulaghai, ubadhirifu na utakatishaji fedha na kuhusika katika sakata kubwa ya kifedha nchini Msumbiji.



Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii