Mfalme Charles III na mkewe Malkia Consort Camilla wapondwa na mayai wakati wakiwa kwenye ziara ya kaskazini mwa Uingereza.
Kisa hicho kilitokea wakati umati wa watu ulikusanyika kwenye eneo la Micklegate, mlango wa kitamaduni wa kifalme wa jiji, kuwasalimu wanandoa hao.
Mfalme huyo walipigwa na mayai matatu ambayo yalitua karibu yao wakati wa matembezi ya ziara hiyo.
Charles alikuwa akisalimiana na watu mashuhuri ghafla mayai yalirushwa kuelekea kwake na alitulia kwa muda kidogo ndipo watu wakaangalia na kukuta mayai yamepasuka chini.
Wakati tukio hilo likitokea, mwanamume mmoja alisikika akipiga kelele akisema "nchi hii ilijengwa kwa damu ya watumwa" na "sio mfalme wangu" kabla ya kuzuiliwa na maafisa kadhaa wa polisi kutokana na picha zilizoenea mitandaoni.
Mwandamanaji huyo pia aliwazomea wanandoa hao wa kifalme kabla ya kuonekana akiwarushia mayai na halikadhalika alikamatwa na polisi na kuwekwa kizuizini.