Ousmane Sonko, mwenye umri wa miaka 48, alishtakiwa mwaka jana kwa kumbaka mfanyakazi wa saluni ambapo alikuwa akifanyiwa masaji.
Kukamatwa kwake na kufunguliwa mashtaka mnamo mwezi Machi 2021 kulisababisha ghasia mbaya za siku kadhaa nchini Senegal, taifa ambalo kwa kawaida linatazamwa kama mwanga wa utulivu katika eneo la Afrika Magharibi lenye hali tete ya kisiasa.
Sonko anadai Rais wa Senegal Macky Sall anajaribu kutega mtego kwa ajili yake na wafuasi wake na Jumatano aliomba utulivu, akiwataka kutokukusanyika nje ya mahakama.
Kesi ya Alhamisi katika mji mkuu wa Senegal ilidumu kwa saa tatu. Usalama mkubwa uliwekwa katika jiji lote, haswa karibu na nyumba ya Sonko na jengo la mahakama.