Korea Kaskazini yafyatua makombora, ikiwa ni pamoja na la masafa marefu

Korea Kaskazini imefyatua makombora kadhaa mapema hii leo ikiwa ni pamoja na linalohisiwa kuwa la masafa marefu hatua iliyoibua mashaka kwa wakazi wa maeneo ya kaskazini na katikati mwa Japan waliotoa mwito wa hifadhi.

Maafisa wa Korea Kusini na Japan wamesema kombora hilo lililopita Japan huenda likawa la masafa marefu, ICBM moja ya silaha za masafa ya mbali za Korea Kaskazini zilizoundwa kubeba vichwa vya nyuklia hadi maeneo mengine ya dunia.

Korea Kaskazini pia ilifyatua angalau makombora mawili ya masafa mafupi. Hatua hii inakuja siku moja baada ya taifa hilo kufyatua karibu makombora 23 idadi kubwa kabisa kwa siku kuwahi kushuhudiwa ikiwa ni pamoja na kombora moja lililotua kwa mara ya kwanza kwenye pwani ya Korea Kusini.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii