Kiwanda Cha Iphone Bandia Chagunduliwa Msumbiji

Mamlaka zimegundua uwepo wa Kiwanda haramu kinachotengeneza Simu za Kampuni ya #AppleInc bandia katika Mji Mkuu Maputo, ambapo walinasa Simu 1,165

Kiwanda hicho kinachomilikiwa na Raia wawili wa #China, kiliweza kutekeleza taratibu za kiufundi wa Simu, kama kuunganisha (Assembly) na kugawa namba za IMEI, ambayo hurahisisha utambuzi wa uhalali wa Kifaa

Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Forodha, Gino Jone, amesema kuna tuhuma kwamba baadhi ya Simu za Mkononi huenda zimeibiwa kwasababu hakuna hati inayohalalisha uingizwaji na uuzwaji wao Sokoni.


Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii