Wanafunzi watatu wafariki dunia bweni likiteketea

Wanafunzi watatu wa Shule ya Msingi Buhangija Manispaa ya Shinyanga wamefariki dunia huku 29 wakinusirika baada ya bweni walilokuwa wamelala kuteketea kwa moto.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Shinyanga, Janeth Magomi amethibitisha kutokea tukio hilo huku akisema moto huo uliyoteketeza bweni la wasichana la shule hiyo umezuka saa 5 usiku wa jana Jumatano, Novemba 24, 2022.


"Moto huo umeanza kuwaka usiku wakati wanafunzi hao wakiwa wamelala ndani ya bweni ambapo idadi yao walikuwa 32 waliokuwa ndani wengine wameokolewa," amesema Magomi

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii