DRC yatumia ndege za kivita na vifaru dhidi ya waasi wa M23

Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo imetuma jana ndege mbili za kivita ili kukabiliana na wanamgambo wa M23 wanaoendelea kusonga mbele katika eneo la mashariki mwa nchi hiyo lenye hali tete, baada ya jumuiya ya kikanda kuwataka waasi kuweka chini silaha.Vifaru na ndege mbili za kivita zililenga maeneo kadhaa ya waasi katika mji wa Kibumba. Katika wiki za hivi karibuni.

waasi wa M23 wamekuwa wakizidi kusogea kuelekea mji wa Goma ambao ni muhimu kibiashara kwa watu milioni moja mpakani mwa Rwanda. Jumuiya ya nchi za Afrika Mashariki imetoa wito wa mazungumzo ya amani katika mji mkuu wa Kenya Nairobi mnamo Novemba 21.

Zaidi ya makundi 120 yenye silaha yanaripotiwa kote mashariki mwa Kongo, ambayo mengi yametokana na athari za vita vya kikanda ambavyo vilipamba moto mwanzoni mwa karne hii.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii