POPO WAVAMIA KITUO CHA POLISI

Maafisa katika Kituo cha Polisi cha Maragua, Kaunti ya Murang'a wanaishi kwa hofu baada ya maelefu ya popo kuvamia kituo hicho. 


Maafisa hao wa usalama wamesimulia masaibu ya kuvamiwa na popo wengi usiku na mchana, huku juhudi za Huduma kwa Wanyama Pori (KWS) kuwatoa lakini waliambulia patupu.

"Nimesikia wenyeji wengine wakitushutumu kwa kumiliki popo hawa. Wanasema wako hapa kutulinda dhidi ya nguvu za giza," alisema Chief Warden wa Kaunti ya Murang'a Laurence Chege .

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii