Korea Kaskazini yafyatua kombora lingine

Korea Kaskazini mapema leo imerusha kombora la masafa mafupi kuelekea katika bahari yake ya Mashariki na pia kutuma ndege za kivita karibu na mpaka na Korea Kusini, na kuongeza zaidi uhasama uliochochewa na majaribio kadhaa ya silaha ya hivi majuzi ya Korea Kaskazini.

Jeshi la Korea Kusini pia limesema liligundua Korea Kaskazini ikifyatua takriban bunduki 170 za kurusha makombora kutoka maeneo ya Pwani ya Mashariki na Magharibi karibu na eneo la mpaka na kwamba makombora hayo yalianguka ndani ya maeneo ya kinga ya bahari ambayo Korea hizo mbili zilianzisha chini ya makubaliano ya kijeshi ya mwaka 2018 ya kupunguza mvutano.

Hatua za Korea Kaskazini zinapendekeza kwamba itaendelea na harakati za uchokozi za majaribio ya silaha yanayonuia kuimarisha uwezo wake wa nyuklia kwa sasa.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii